top of page

MADA ZA KISWAHILI - KIDATO CHA NNE

MADA 1: Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

 

 1. Uundaji wa Maneno

  • Elezea njia mbalimbali za uundaji maneno

  • Elezea mazingira yanayoelezea kuhitaji maneno mapya

  • Unda maneno katika miktadha mbalimbali

 

MADA 2: Ukuaji Na Ueneaji Wa Kiswahili Enzi Ya Waingereza Na Baada Ya Uhuru

 

 1. Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili katika enzi ya Waingereza

  • Elezea mambo waliyochangia waingereza katika ukuaji wa Kiswahili nchini Tanzania

 2. Ukuaji na Ueneaji wa Kiswahili baada ya Uhuru

  • Elezea shughuli mbalimbali zinazowezesha kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini

  • Elezea dhima ya kila asasi inayokuza Kiswahili

 

MADA 3: Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

 

 1. Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya

  • Fafanua vipengele vya uhakiki

  • Baini taarifa muhimu za mwandishi wa kila kitabu

 

MADA 4: Kutunga Kazi Za Fasihi Andishi

 

 1. Utungaji wa Mashairi

  • Fafanua mambo ya kuzingatia katika utungaji wa mashairi

 

MADA 5: Uandishi

 

 1. Uandishi wa Insha za Kiada

  • Elezea muundo wa insha za kaida

 2. Uandishi wa Hotuba

  • Elezea muundo wa hotuba

 3. Uandishi wa Risala

  • Elezea muundo wa risala

 4. Uandishi wa kumbukumbu za Mikutano

  • Elezea mambo ya kuzingatia katika uchukuaji wa kumbukumbu za mikutano

 

MADA 6: Ufahamu

 

 1. Ufahamu wa Kusikiliza

  • Jibu maswali ya habari uliyosikiliza

  • Fupisha habari

 2. Ufahamu wa Kusoma

  • Jibu maswali kutokana na habari ndefu uliyosoma

  • Fupisha habari ndefu uliyosoma

bottom of page