top of page

KUFUNGULIWA KWA SHULE

TAARIFA KWA WAZAZI, WALEZI NA WANAFUNZI WOTE 


KUFUNGUA SHULE 

  1. Shule itafunguliwa na kuanza masomo kwa vidato vyote  siku ya JumaMOSI tarehe 10/01/2024. Mwanafunzi anatakiwa kuwa amesharipoti shuleni ili asikose vipindi, 

  2. Wanafunzi wa Bweni wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia siku ya Jumatano tarehe 10/01/2024, ambapo zimetengwa siku mbili maalumu za kupokea wanafunzi ambayo ni Jumatano tarehe 10/01/2024 na Alhamisi ya tarehe 11/01/2024 kuanzia saa mbili kamili subuhi mpaka saa kumi na moja jioni. Hakuna mwanafunzi atapokelewa zaidi ya saa kumi na moja jioni, na tumeongeza siku ya Alhamisi kupokea wanafunzi ili kupunguza msongamano. 

  3. Mwanafunzi aletwe shuleni na mzazi/mlezi mmoja ili kuepusha msongamano, na mwanafunzi ahakikishe amejibu maswali yote aliyotumiwa kufanya kipindi cha likizo. Ambae atakuwa hajamaliza maswali yote HATOPOKELEWA

  4. Kwa siku za kawaida, ofisi za shule ziko wazi kwa huduma kuanzia Jumatatu mpaka Jumamosi, saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni. Wazazi/walezi walio maeneo jirani mnashauriwa kufika shuleni na kukamilisha taratibu za usajili na kupata clearance kwa mwanafunzi siku yoyote kuanzia leo, ili siku ya kuripoti kupunguza msongamano. 


MKUU WA SHULE 

14/11/2023.


KUFUNGULIWA KWA SHULE
bottom of page